Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.
KAMPUNI ya Megatrade Investiment Ltd ya jijini Arusha imekabidhi zawadi katika kituo cha kulelea watoto yatima na waishio katika mazingira magumu cha Kili Center kwa ajili ya msimu wa siku kuu za mwisho wa mwaka.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zwadi hizo meneja mauzo na masoko wa Megatrade Goodluck Kway alisema msaada huo ni sehemu ya faida iliyopatikana kutokana na utumiaji wa kinywaji cha K-Vant Gin hivyo kampuni ikaonelea ni vyema ikarejesha kwa jamii hususani watoto waishio katika mazingira magumu.
Alisema Mega trade investment ltd imetoa zawadi ya kilogram 50 za mchele, kilogram 100 za Unga wa Sembe,kilogramu 50 za unga wa ngano.kilogramu 75 sukari na kwa ajili ya kupikia lita 50.
Vitu vingine ni Katoni mbili za sabuni za kufulia,Dawa za meno,Mafuta ya kupaka mwilini,Vinywaji vya aina tofauti sanjari na madaftari kwa ajili ya maandalizi ya mwaka mwingine wa masomo utakao anza January mwakani .
“Megatrade tunatambua kuwa watoto yatima pia wanayo haki ya kusherehekea siku kuu za Krismas na mwaka mpya kama walivyo watoto wenzao na ndio sababu tumekuwa na utaratibu wa kuwapatia msaada kila mara pindi tunapo pata nafasi”alisema Kway.
Aliziomba taasisi nyingine na makampuni mbalimbali kujitokeza kulisaidia kundi hilo ambalo hivi sasa linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosekana kwa vifaa vya shule hususani kwa watoto wanao bahatika kuendelea na masomo.
Akizungumza kwa niaba ya watoto wenzake Neema Omary aliishukuru kampuni ya Megatrade kwa kuwakumbuka kwa msaada huo huku wakiendelea kutoa wito kwa watu binafsi na makampuni mengine kujitokeza kutoa msaada ambao utawasaidia katika shughuli zao mablimbali za kimaendeleo.
Posted by
Unknown
0 Response to "MEGATRADE YA JIJINI ARUSHA YAWAKUMBUKA WATOTO YATIMA WA KITUO CHA KILI CENTER CHA MOSHI"
Post a Comment