Home » Uncategories » DUH..BAADA YA LILE SKENDO LA KUJIUZA...BABY MADAHA ATI ATANGAZA KUACHA MUZIKI....!!
Thursday, 20 February 2014
DUH..BAADA YA LILE SKENDO LA KUJIUZA...BABY MADAHA ATI ATANGAZA KUACHA MUZIKI....!!
IKIWA imepita miezi kadhaa tangu anaswe katika mtego wa kujiuza na
makachero wa OFM ya Global Publishers, staa wa Bongo, Baby Madaha
ametangaza kuachana na sanaa ya muziki na filamu kwa maelezo kuwa
amechoshwa na maisha ya presha.
Akistorisha na paparazi wetu juzikati jijini Dar es Salaam, Madaha
alisema ishu ile imemsababishia matatizo makubwa ya kifamilia na hata
kibiashara, hivyo kujutia mchezo mzima ulivyokuwa. Alisema filamu anayoisambaza kwa sasa na kibao chake cha mwisho
kukitoa cha Mr. Dj ndizo zitakazofunga pazia la mambo ya sanaa kwa
upande wake.
“Nimeamua
kuachana na sanaa kabisa, siwezi kuishi maisha ya presha yasiyo na
uhuru. Nitarudi kwenye fani yangu niliyosomea (hakutaka kutaja), maana
naishi maisha ambayo hayana amani kabisa,” alisema.
Hivi karibuni Madaha aliingia kwenye kumi na nane za Oparesheni
Fichua Maovu ‘OFM’ ya Global Publishers ambapo alipatana bei ya kutoa
uroda kwa ‘mfanyabiasha’ wa madini kutoka jijini Mwanza
aliyejitambulisha kwa jina la Mike – kumbe ulikuwa mtego....
0 Response to "DUH..BAADA YA LILE SKENDO LA KUJIUZA...BABY MADAHA ATI ATANGAZA KUACHA MUZIKI....!! "
Post a Comment