Msanii chipukizi wa filamu wa Kundi la Mwamba Arts, Mariam Glant.
MSANII chipukizi wa filamu wa Kundi la Mwamba Arts, Mariam Glant (20)
amenusurika kifo baada ya kunywa sumu kisa kikidaiwa kuwa ni penzi la
kijana aliyejifanya mdogo wa Kanumba anayejulikana kwa jina moja la
Chief.
Akizungumza na paparazi wetu sosi wa
karibu na msanii huyo alisema siku ya tukio, Mariam alikuwa nyumbani kwa
rafiki yake wa kike maeneo ya Mbezi Mwisho, jijini Dar ambapo rafiki
yake huyo alitoka kidogo na kumuacha peke yake nyumbani hapo.
Sosi huyo alisema baada ya muda
mfupi alitumiwa ujumbe mfupi wa maneno kutoka kwa Mariam ukisema ‘mimi
ndiyo nakufa hivyo nimekunywa sumu.’
Baada ya rafiki huyo kupata
ujumbe huo, alirudi nyumbani haraka na kumkuta Mariamu akiwa amezimia
huku akitokwa na mapovu mdomoni ambapo kwa kushirikiana na wasamaria
wema walimchukua na kumkimbiza kituo cha polisi kuchukua PF3 na
kumpeleka hospitali ya tumbi ambapo alipatiwa matibabu.
Akielezea
kwa uchungu baada ya kupata ahueni, Mariam alisema yeye na mpenzi wake
huyo waligombana siku chache kabla hajachukua uamuzi wa kunywa sumu.
“Sababu kubwa iliyonifanya ninywe
sumu ni huyo mwanaume kwa sababu kwanza alinidanganya yeye ni mdogo wake
Kanumba na nikiwa naye kimapenzi atanitoa kisanaa na nitakuwa maarufu
lakini baada ya kuingia kwenye uhusiano hakunisaidia chochote zaidi
nilikuja kugundua kwamba hana hata undugu na Kanumba tukagombana,”
alisema Mariam aliyeng’ara katika sinema za Mwanamipango Comedi, Gods
Kingdom na M23.
Saturday 25 January 2014
0 Response to " KANUMBA ASABABISHA MSANII WA BONGO MOVIE SUMU KISA PENZI LAKE."
Post a Comment