YANGA WAMKATIA RUFAA MCHEZAJI WA MGAMBO MOHAMED NETO

YANGA SC imekata rufaa dhidi ya mchezaji Mohammed Neto wa Mgambo Shooting ikidai anacheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kinyume cha kanuni za usajili. Yanga SC wanalalamikia usajili wa mchezaji huyo una mapungufu kwa kuwa ni raia wa kigeni, lakini hana Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC).
Ubingwa mezani? Kikosi cha Yanga iliyokata rufaa kutaka kukombo pointi ilizopoteza kwa Mgambo 
Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Evodius Mtawala amekiri kupokea rufaa ya Yanga SC, lakini hakuwa tayari kuzungumza zaidi. “Ndiyo tumepokea, ila nipo kwenye kikao siwezi kuzungumza zaidi,”alisema Mtawala, anayekaimu nafasi ya Celestine Mwesigwa aliye Afrika Kusini kwa sasa. Dhamira ya Yanga SC kutaka rufaa hiyo inaweza kuwa kukomboa pointi walizopoteza kwa Mgambo JKT Jumapili iliyopita kwa kufungwa mabao 2-1 Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu. Lakini kwa mujibu wa kanuni za sasa za Ligi Kuu, baada ya usajili hutolewa muda maalum wa pingamizi kwa wachezaji na anapopitishwa hata ikikatwa rufaa, haibadili matokeo zaidi mchezaji au kiongozi aliyefanya udanganyifu kuchukuliwa hatua.
Mohamed Neto wa Mgambo JKT akichuana na William Lucian 'Gallas' wa Simba katika Ligi Kuu msimu huu mechi ya mzunguko wa kwanza.Mchezaji huyo amekatiwa rufaa na Yanga
Lakini pia katika utaratibu wa sasa wa usajili, kila mchezaji mpya katika Ligi Kuu anatakiwa kuwasilisha ama cheti cha kuzaliwa au hati ya kusafiria- ambavyo pamoja na kusaidia umri wa mchezaji kujulikana pia huainisha uraia wake. Neto alicheza kwa dakika 30 tu mechi dhidi ya Yanga baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu. Alipewa kakadi ya njano ya kwanza akikataa kukaguliwa na refa Alex Mahagi na ya pili kwa kuzozana na refa huyo akipinga kusachiwa kama amebeba hirizi. Yanga SC inahaha kuhakikisha inafufua matumaini ya kutetea ubingwa wake na sasa inahamishia nguvu zake mezani, baada ya mambo kuwaendea kombo uwanjani na kuachwa na Azam FC katika mbio hizo. Azam FC inaongoza kwa pointi zake 53 baada ya kucheza mechi 23, ikifuatiwa na Yanga SC yenye pointi 46 za mechi 22 na Mbeya City yenye pointi 45 za mechi 23 ni ya tatu.

0 Response to "YANGA WAMKATIA RUFAA MCHEZAJI WA MGAMBO MOHAMED NETO "

Post a Comment

wdcfawqafwef