AIBU:MAPICHA YA FUMANIZI:MWALIMU WA CHUO CHA TRA AFUMWANA NA MCHUMBA WA MTU GETO KWAKE

Mhadhiri wa Chuo cha Kodi ya Mapato Tanzania, Richard Donati amezuliwa timbwili la aina yake nyumbani kwake, hali iliyosababisha mtaa kufungwa, kisa kikielezwa ni kukutwa na mchumba wa mtu aliyetajwa kwa jina moja la Aisha.


Mwenye mchumba (kushoto) akitulizwa baada ya kupandisha hasira.
HABARI KAMILI
Sakata hilo lilitokea mchana kweupe, Ijumaa iliyopita,  Sinza – Kwa Remmy jijini Dar es Salaam ambapo timu ya mapaparazi wetu ilishuhudia mchezo mzima baada ya kupigiwa simu na mmoja wa mashuhuda walioona dalili za vurugu tangu mapema.
Shuhuda: “Jamani hapo si OFM (Oparesheni Fichua Maovu)?”
OFM: “Ndiyo penyewe ndugu, tuambie.”
Mhadhiri wa Chuo cha Kodi ya Mapato Tanzania, Richard Donati (wa kwanza kushoto) baada ya tukio hilo.
Shuhuda: “Kuna jamaa yuko hapa mtaani kwetu Sinza-Kwa Remmy, amemfuata demu wake kwa mshkaji mmoja hivi, ni ticha wa Chuo cha Kodi ya Mapato Tanzania, njooni haraka maana anamsubiri jamaa amtoe ndiyo amchukue demu wake. Yupo hapa getini,” alisema shuhuda huyo.
KUMBE NI MWANAFUNZI WAKE!
Ndani ya dakika 15, OFM wakawa wamefika eneo la tukio  na kukutana uso kwa uso na aliyedai ni mwenye mali ambaye alijitambulisha kwa jina moja la Ibra.
Alisema alikuwa eneo la tukio kwa ajili ya kumchukua mchumba wake ambaye anatembea na mwalimu wake huyo.
Wananchi wakilizonga gari alilokuwemo mchumba wa mtu.
“Tangu asubuhi ameingia humu ndani, simu amezima ili nisimpate. Ndugu zangu naonewa, mimi nimetoka mbali na mchumba wangu, nimeshaanza baadhi ya taratibu nyumbani kwao. Najulikana kila mahali, naye anajulikana kwetu, lengo langu ni kumuoa, lakini jamaa anaamua kutumia ualimu wake kumdanganya mchumba wangu.
“Mimi najua anatumia mwanya wa kuwa mwalimu wake ili kumfaidi. Mchumba wangu anaogopa kumkataa kwa sababu anaweza kumfelisha chuoni, naijua sana hiyo michongo,” alisema Ibra ambaye alikuwa akizungumza kwa hisia kali, wakati mwingine machozi yakimtoka.
Mchumba wa mtu akizidi kutulizwa na rafiki yake.
MWENYE MALI, TICHA WAZOZANA
Ibra akiwa ameambatana na mjumbe wa shina aliyetajwa kwa jina la mama Kibibi na wapambe wengine waliokuwa eneo la tukio, walifika getini kwenye nyumba ya mwalimu huyo na kugonga, lakini kabla mlango haujafunguliwa, gari aina ya Toyota Harrier lilifika getini hapo na dereva akapiga honi, geti likafunguliwa, gari likaingia ndani.
Muda mfupi baadaye mwalimu huyo alitoka ndani na kuhoji uhalali wa Ibra kwenda nyumbani kwake huku akidai hana mamlaka ya kumfuata kwa kuwa msichana yule ni mchumba tu na si mke.
Wananchi wakiwa eneo hilo la timwili.
Majibizano yalichukua nafasi kubwa kabla ya Donati kukimbia ndani na kwenda kujigonga kwenye ukuta jambo lililosababisha apasuke usoni na kuanza kuvuja damu.
Tukio hilo lilionekana kumchanganya sana Donati na muda mfupi baadaye alitoka mbio na kuelekea kusikojulikana.
IBRA, AISHA USO KWA USO
Aisha aliyekuwa ndani ya gari akiwa amekaa siti ya dereva (alihama kutoka siti ya nyuma) alipata nafasi ya kuzungumza na Ibra ambaye alimsihi ashuke ili waende nyumbani kwa wazazi wa binti huyo kutafuta suluhisho.
Hata hivyo, msichana huyo alisikika akisema: “Ibra siwezi kushuka hapa. Aibu yote hii? Watu wamejaa hivyo, nitashukaje? Sishuki kwa kweli.”
WANANCHI WAJA JUU
Umati uliokuwa eneo la tukio ulikuja juu ukimtaka rafiki wa mwalimu Donati (yule aliyefika na Harrier) amfungulie mlango Aisha ili aondoke na Ibra jambo ambalo halikuzaa matunda hata kidogo.
Hata hivyo, kuna wakati jamaa huyo alimwita Ibra pembeni na kuzungumza naye wawili matatu na kisha Ibra kuamua kuondoka zake.
IBRA NYUMA YA NONDO
Habari zilizopatikana wakati Wikienda linakwenda mitamboni zinaeleza kuwa, Ibra alikamatwa na askari na kufikishwa katika Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar. Inadaiwa alikamatiwa nyumbani kwa akina Aisha (hakukutajwa jina) ambapo alikwenda kwa lengo la kusuluhishwa na wazazi wa binti huyo.

0 Response to "AIBU:MAPICHA YA FUMANIZI:MWALIMU WA CHUO CHA TRA AFUMWANA NA MCHUMBA WA MTU GETO KWAKE "

Post a Comment

wdcfawqafwef