Picha
za nusu utupu ambazo amezipiga mwanamitindo maarufu Bongo, Jokate
Mwegelo zinaonekana kumtesa kufuatia baadhi ya waumini wa kanisa
analosali kumsema kuwa
anakwenda kinyume na maadili.
Picha hizo anazoonekana amevaa gauni refu jekundu huku likiwa na mpasuo ‘wa haja’
uliyolifanya sehemu kubwa ya paja lake kuwa wazi, zimesambaa kiasi cha
kuwafanya baadhi ya mashabiki wake kumtaka ajiangalie upya. Wakizungumza
na Ijumaa kwa nyakati tofauti, baadhi ya wadau wamesema kutokana na
jinsi alivyokuwa ametulia kiimani, mrembo huyo alikuwa anaelekea kwenye
ulokole lakini kwa hili anapotea.
“Unajua
yule ni modo mwenye jina kubwa sana lakini alikuwa ametulia sana, hata
nilipomuona amejiunga na kwaya ya pale kanisani kwetu St. Peter, niliona
ameamua kumfuata Yesu kikwelikweli lakini kwa picha hizi, mh!” alisema Juster John anayesali kanisani hapo.
Naye rafiki wa Jokate aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema: “Ninachokumbuka
Jokate aliwahi kuniambia anataka kuokoka ili amtumikie Yesu kisawasawa
lakini kwa mavazi haya nadhani mawazo ya ulokole itakuwa basi tena.”
Ijumaa lilifanya jitihada za kumtafuta Jokate na kumuuliza juu ya picha hizo, alipopatikana alisema: “Nilizipiga kwa ajili ya kuitangaza kampuni yangu ya mitindo ya Kidoti.
Ijumaa: Sasa mbona umeacha mapaja wazi sana?
Jokate: Huh! Ijumaa: Huh nini?
Jokate: Nishasema ni za Kidoti, ilikuwa ni kwa ajili ya kutangaza nguo na nywele zangu.
Ijumaa: Kuokoka ndiyo basi tena?
Jokate:
Kimyaaa. Hata hivyo gazeti hili linamshauri mrembo huyu kwamba, kwa
kuwa ameshajijengea heshima kubwa kwenye jamii, ni vyema akawa makini na
mavazi kama haya ambayo yanaweza kumfanya akatafsiriwa tofauti.
>>GPL
Saturday, 1 March 2014
0 Response to "PICHA ZA UTUPU ZA JAKATE ZAZUA GUMZO KANISANI KWAKE ANAKOSALI, WAUMINI WENZAKE WAKERWA NA KITENDO HICHO...SOMA ZAIDI HAPA"
Post a Comment