Mimi
ni mama wa miaka 36, nina watoto watatu, nina miaka tisa kwenye ndoa,
tulipoona na mume wangu tulikuwa tukifanya mapenzi style za kawaida tu,
tunabadili style lakini ni zile za kawaida
Umefika
miezi sasa mume wangu amebadilika sana, yani hatulii yani mimi nayeye
hatukai nusu saa bila ugomvi, kitu kidogo tu, hasira kwangu na anapeleka
hadi kwa watoto wangu, yani hadi wanamuogopa sasa hivi, wakimuona tu!
Wote wanaenda kulala,
Hadi
sasa nahisi mume wangu anamwanamke nje, tena ni Malaya kabisa, maana
mume huyu huwa nakaa namfikiria naona kama wamenirogea vile, hajui
kubembeleza kwenye mapenzi, yeye ni kuamrisha tu, tofauti na zamani,
hata mimi nikimbembeleza labda nimshike shike sehemu ambazo najua
akishikwa anafurahi, nimnyonyenyonye hapa na pale, zamani alikuwa
anapenda sana. Siku hizi hataki kabisa, nikianza tu, anasema ah!
Nimechoka mimi, kwanza nimeshaoga unanipaka matemate yako, wakati bafu
liko hapo chumbani angeweza kuoga tena,
Sasa
kuna kipindi nami niliamua kukaa kimya, nikawa nasubiri hadi yeye
aanze, lakini sasa style alizokujanazo sasahivi mimi siziwezi, yani sio
za kawaida, nina mwili mkubwa, nilizaa kwa operation, nina kovu tumboni,
siwezi kujikunja kunja Napata maumivu, sasa yeye utakuta ananikunja
kama samaki, yani nabanwa nakuwa mdogo, nalia sana, sio kwa raha ila ni
kwamaumivu, na hata nikilia anasema nisubiri hadi amalize ndio aniache,
akiniacha tu! Ujuwe lazima nitalala hata siku mbili, naumwa sana kiuno,
Kuna
siku nilimuuliza kwanini ananifanya kama ananibaka vile, akasema
akifanya style za zamani hasikii raha kabisa, kuna kipindi alianza
kuniambia kuwa anataka anifanye nyuma, sikuamini masikio yangu, nililia
sana, nikamwambia ndoa na ife, narudi kwetu, akanisihi nibaki, nashukuru
hakurudia tena kutamaka ushenzi huo,
Style
zake za sasa hivi sijui anazitoa wapi, yani sasahivi akiniambia kama
anahitaji tu! Basi naweza meza hata dawa ili nijifanye naumwa, napoteza
furaha kabisa, yani hawezi kabisa kunifanya kawaida, naombeni mnishauri
nifanyaje, maana ni kweli kwa mwanamke yeyote Yule style ninazofanywa
mimi, lazima angelia, mimi hadi huwa nakwenda hospitali, ila nikifika
sisemi kama nimefanya style mbaya, huwa nadanganya maana naona ni aibu,
nitamuaibisha mume wangu na mimi pia.
Saturday, 1 March 2014
0 Response to "JAMANI MUME WANGU ANATAKA STYLE ZA MAPENZI ZA AJABU AJABU, ZINANIUMIZA… USHAURI JAMANI NIFANYEJE...?"
Post a Comment