AFISA MSTAAFU WA NMB AFARIKI DUNIA KWENYE AJALI YA BASI NA TRENI

DSC06845
Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Manyoni, Dk.Kitundu Jackson ,akitoa maelezo kwa waandishi wa habari juu ya mapokezi ya majeruhi wa basi la bunda lililogonga kichwa cha Treni leo.Picha zote na Nathaniel Limu.
DSC06809
Bbasi la Bunda lililokuwa likitokea mjini Dodoma linakwenda jijini Mwanza na kugonga kichwa cha Treni maeneo ya mjini Manyoni,linavyoonekana katika picha baada ya kugonga.
DSC06818
Baadhi ya majeruhi wa basi la Bunda lililogonga kichwa cha Treni mjini Manyoni,wakiwa wanapatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Manyoni.
DSC06819
Na Nathaniel Limu, Manyoni.

AFISA Mstaafu wa NMB benki tawi la Manyoni mkoani Singida ambaye kwa sasa alikuwa Mhasibu wa SACCOS ya chama cha walimu Tanzania Manyoni,Belida Kombo amefariki dunia baada ya basi la kampuni ya Bunda alilokuwa akisafiria kugonga kichwa cha treni na kujeruhi abiria wengine 39.

Basi hilo T.782 BKZ aina ya scania lililokuwa Farak Adamu lilikluwa likitokea Dodoma mjini kuelekea jijini Mwanza,liligonga kichwa cha treni eneo la makutano ya barabara kuu ya Dodoma – Singida na reli eno la round about ya Manyoni mjini leo saa moja na nusu asubuhi.

Bi Kombo ambaye alipandia basi hilo katika kituo cha mabasi cha Manyoni mjini na alifariki dunia dakika chake wakati akihangaika kutafuta kiti.Pia ndugu zake waliomsindikiza wakiwa bado hawajaondoka eneo lam kituo cha mabasi.

Akizungumza na waandishi wa habari Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Manyoni,Dk.Kitundu Jackson amekiri kwamba amepokea majeruhi 39 wa ajali ya treni na basi na kati yao sita wana hali mbaya. Amesema majeruhi walio na hali mbaya ni pamoja na kondakta wa basi Masage Bunyema na kwamba baadhi watapewa rufaa ya kupelekwa hospitali ya mkoa wa Dodoma na wengine katika hospitali ya misheni ya St.Gasper Itigi.

“Tayari majeruhi wawili tumeisha wapa rufaa kwenda kupata matibabu katika hospitali ya mkoa ya Dodoma mjini na sista mmoja tumempeleka katika hospitali ya misheni ya St.Gasper Itigi”,alifafanua zaidi Dk.Kitundu.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Manyoni,Fatma Toufiq ameiangiza mamlaka ya TRL na TANROADS kujenga haraka kuweka mtumishi wa kutoa angalizo kwa vitambaa juu ya gari la moshi linapopita katika eneo hilo ambali kumetokea ajali tatu katika kipindi kifupi kilichopita.

Aidha,mashuhuda wa ajali hilo,wamedai kuwa hicho kichwa cha treni kilichokuwa kikitokea katika kijiji cha Aghondi,dereva wake alijitahidi kupiga honi kali ili kumwonya dereva wa bunda basi lakini dereva huyo hakujali.Kama haitoshi,dereva wa hiece aliyekuwa apishane na basi hilo,alimumulika kwa taa akimwonya asimame ili kipisha kichwa hicho,lakini hakujali pia.

Watu hao wamedai kuwa dereva wa basi hilo alikuwa kwenye mwendo kasi wakati akipewa onyo hilo la kupisha kichwa cha treni lipite.

0 Response to "AFISA MSTAAFU WA NMB AFARIKI DUNIA KWENYE AJALI YA BASI NA TRENI "

Post a Comment

wdcfawqafwef