Siku
za nyuma, wanaume walijali zaidi uzuri wa sura na mwili wakati
walipokuwa wanatafuta mke. Lakini utafiti uliofanywa duniani kote
unaonesha kwamba, wanaume hivi sasa wamebadili mitazamo na kuanza
kuangalia vitu vilivyo zaidi ya uzuri wa sura na mwili. Watafiti kutoka
Chuo Kikuu cha Grand Valley kilichopo jimboni Michigan nchini Marekani
walioendesha sehemu kubwa ya utafiti huo wamesema,
wanaume hivi sasa wameanza kujali uwezo wa wanawake
katika kufikiri na kujua namna ya kujenga maisha kuliko kujali sura zao
na maumbile.
Tafiti nyingi, ukiwemo huo wa karibuni wa Chuo cha Grand Valley,
zinaonesha kwamba, kwenye miaka hadi 1980, wanaume walikuwa wakioa wake
ambao wanaume hao wanawazidi kielimu na hata kimapato. Lakini kufikia
mwaka 2002, wanaume wengi walikuwa wameoa wanawake ambao wanawazidi
kielimu, kimapato au kukaribiana.
Lakini pia imebainika kwamba, hadi kufikia miaka hiyo, wanaume na jamii
nyingi zilikuwa zikimtazama mwanamke anayefaa kuolewa kuwa ni yule mzuri
sana kwa sura na umbo. Lakini kufikia mwaka 2002, wanaume wengi na
jamii walikuwa wanaamini kwamba, mwanamke mwenye uwezo mkubwa wa kuelewa
maisha ndiye anayefaa kuwa mke.
Kwa miaka ishirini hali imebadilika sana. Maisha yamezidi kuwa magumu na
uhitaji wa watu kusaidiana katika kuyakabili umeongezeka. Kwa hiyo mtu
anapofikiria kuoa huanza kujiuliza atakavyomudu maisha na mke. Kwa hofu
za kushindwa, hujikuta akijiuliza namna atakavyoweza kusaidiana na huyo
anayetaka kumwoa katika kufanya mambo yaende.
Siku za nyuma, mwanamke mwenye kipato kizuri alikuwa katika ugumu wa
kupata mume, lakini siku hizi, bila kujali sura au sifa nyingine,
uhakika wa mwanamke kuwa na njia za kipato unampa, nafasi kubwa zaidi ya
kuolewa. Kilichokuwa kinaogopwa huko nyuma na wanaume kwa sasa ndicho
kinachokimbiliwa.
Tafiti hizo zinasisitiza kwamba, thamani ya mwanamke kwenye jicho la
mwanaume inaanza kuondoka kwenye uzuri wake wa sura na mwili na kuingia
kwenye uwezo wake katika kuyakabili maisha. Hii ikiwa na maana kwamba,
kwa kadiri siku zinavyoenda, wanawake ambao watakuwa na nafasi kubwa ya
kuolewa watakuwa ni wale waliosoma au wale wenye shughuli za kuzalisha.
Wataalamu wengi wanasema, hivi sasa uzuri unaonekana kabisa
kubadilishana nafasi na elimu na uwezo wa ‘kutafuta maisha’ wa mwanamke.
Kwa hiyo, sasa siyo suala la uzuri tena, bali mwanamke anajua kitu gani
na ana uwezo kiasi gani wa kufanya maisha yawe bora sana.
Hii pia ina maana kwamba, dhana ya zamani ya mwanamke mzuri kuolewa na
mwanaume msomi au mwenye fedha imeanza kukosa mashiko. Siku za nyuma
mwanamke mzuri sana, angeolewa na mwanaume mwenye fedha, kama zilivyo
bidhaa nzuri kuangukia mikononi mwa wenye uwezo kifedha.
Lakini leo hii, wanaume wanachoweza kufanya ni kuwachezea kimapenzi
wanawake wazuri na siyo kuwaoa. Linapokuja suala la kuoa, kisomo na
uwezo wa kuyajua maisha huchukua nafasi. Uzuri wa sura hubaki nyuma
kwanza.
Monday, 17 March 2014
0 Response to " PICHAZ ZA UTUPU MREMBO SASA UAMKE, WANAUME UNAJUA TUNA PENDA NINI?? SOMA HAPA UPATE BAHATI YA KUPENDWA SIO HUO UJINGA WENU "
Post a Comment