
USIOMBE
yakukute! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kusikia kisa cha aliyewahi
kuwa mpenzi wa mwanamuziki wa TAKEU, Nice Lucas Mkenda , Lulu John
(mwenye blauzi nyekundu) anayedai kumfumania mumewe ,
Lulu
alidai kumfumania bwana’ke Abdulatif Salum na mwanamke ambaye jina
halikupatika kwenye gesti moja iliyopo Kinondoni B jijini Dar es Salaam,
mwishoni mwa wiki iliyopita.
SINEMA ILIKUWA HIVI
Kwa
mujibu wa Lulu, akiwa kwenye mihangahiko ya kusaka bingo, alitonywa na
mtu wake wa karibu kuwa mumewe Abdulatif yupo kwenye nyumba hiyo ya
wageni akiigagadua amri ya sita nje ya mkataba.
Lulu,
baada ya kuthibitishiwa kuwa mumewe anacheza ‘nje kapu’ ndipo akakodi
bodaboda fasta na kuwahi eneo la tukio kwani naye siyo mgeni wa uwanja
huo wa mechi za kitandani. Alidai kuwa ilimchukua dakika 12 tu kutoka Kijitonyama, Dar anakoishi na mumewe hadi eneo la tukio.
MPAKA CHUMBANI
Aliendelea
kusema kuwa baada ya kutimba mahali hapo alikwenda moja kwa zote hadi
kwenye chumba walichojichimbia wawili hao na kuanza kubamiza mlango huku
akipiga mayowe ya kuomba msaada.
WENGINE WADHANI WAMEFUMANIWA
Huku
akizidisha kupiga kelele akitaka kuvunja mlango, ndipo akakatiza stimu
za watu wengine waliokuwa wakilimega tunda tamtam kwenye vyumba vingine
ambao walitoka kwa kihoro wakidhani wamefumaniwa wao.
MUME ATIMKA NA NGUO YA NDANI
Aliendelea
kusimulia mkasa kuwa watu walianza kujaa nje ya chumba hicho ndipo
Abdulatif akafungua mlango kwa kasi na kutimka kama mkizi akiwa na nguo
ya ndani pekee kisha akaruka fensi.
WATU WEWEEE!
Alisema
kuwa wakati anachomoka nduki alimgonga kikumbo Lulu na kumwangusha chini
huku akimwacha akigaragara ambapo watu walikuwa wakimkimbiza wakisema:
“Weweee.”
VITA
Baada ya kunyanyuka na Abdulatif kumchomoka hivihivi ndipo vita kuu ikaanza dhidi ya mgoni wake.
ANG’ATWA PUA
Alisema
kuwa ngumi za uhakika zilipigwa hadi yeye (Lulu) akang’atwa pua ambapo
alitokwa na damu chapachapa usoni huku aliyefumaniwa akitafuta njia ya
kujisitiri baada ya kuchaniwa nguo na kubaki mtupu.
Kwa
mujibu wa Lulu, kitendo cha kumfumania mwanaume huyo kimemuumiza kwani
amekuwa akimtunza kwa hali na mali na hakuweza kuamini kama angeweza
kumsaliti. Juhudi za kumpata Abdulatif hazikuzaa matunda hadi gazeti hili linakwenda mitamboni hata hivyo zinaendelea.
KWA NINI USIOMBE YAKUKUTE?
Lilikuwa
ni tukio la aina yake ambalo halikuishia pale gesti tu bali liliingia
mtaani ambapo vitendo vya Abdulatif kukimbia akiwa mtupu na Lulu
kung’atwa pua viligeuka gumzo na kila mtu akimuomba Mungu asikutwe na
kasheshe kama hilo.
0 Response to "MKE AMFUMANIA MUMEWE GUEST BUBU JIONEE MWENYEWE"
Post a Comment