Uchunguzi
uliofanywa nchini Uingereza umeendelea kulipandisha chati umbo la
kibantu, kwa kusema kwamba, kuwa na unene zaidi eneo la mapajani, katika
makalio na katika mahips ni vizuri kiafya, na humzuia mtu asipate
matatizo ya kiafya.
Wataalamu wanasema
kuwa, mafuta yanayopatikana katika mahips, huondoa fati asidi mbaya
kiafya ambazo huwa na mada za kuzuia uvimbe ambazo huifanya mishipa ya
damu isizibe. Timu hiyo ya wachunguzi imesema kuwa, makalio makubwa ni bora kuliko mafuta ya zaida yanayojilundika katika mzunguko wa kiuno, ambayo hayasaidii chochote.
Wachunguzi
hao wamesema katika Jarida la Kimataifa la Obesiti kwamba, sayansi
inapaswa kuangalia jinsi ya kuongeza mafuta katika eneo la mahips na
pengine katika siku zijazo madaktari watatakiwa kuangalia njia za
kuyahamisha mafuta mwilini na kuyapalekea katika sehemu za mahips ili
kulinda afya za watu kutokana na magonjwa ya mishipa ya moyo na magonjwa
mengineyo kama kisukari.
Watafiti hao wameeleza kwamba, kuwa na mafuta kidogo katika hips kunaweza kupelekea matatizo makubwa ya umetaboli.
Wataalamu
hao wameendelea kusema kwamba, ushahidi unaonyesha kwamba, mafuta
yanayozunguka mapaja na sehemu za nyuma ni vigumu kuyeyuka kuliko yale
yaliyo katika kiuno.
Ingawa suala hilo
linaonekama kana kama ni kinyume, lakini ni kweli kwamba kutoyeyuka huko
kuna faida kwani, wakati mafuta yanapoyeyuka kwa urahisi hutoa mada
inayoitwa cytokines ambayo huleta uvimbe katika mwili.Mada za cytokines zinahusiana moja kwa moja na magonjwa ya moyo na kisukari.
Kuyeyuka
taratibu kwa mafuta katika mapaja pia husababisha homoni ya adiponectin
izalishwe kwa wingi na husaidia kudhibiti sukari katika damu na jinsi
mafuta yanavyochomeka.
Dakta Konstantinos Manolopoulos aliyeongoza utafiti huo kutoka chuo kikuu cha Oxford
amesema kuwa, la muhimu ni umbo na wapi mafuta yanakusanyika, na kwamba
unene wa mahips na mapaja ni mzuri kuliko unene wa tumbo.
Sunday, 9 March 2014
0 Response to "MAKALIO MAKUBWA...!!!!SIO KUTAMANISHA TU BALI KUNA VINGI NDANI YAKE...SOMA ZAIDI HAPA... "
Post a Comment