STAA wa mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amedhihirisha kuwa ni
sikio la kufa baada ya kusema yeye ni miongoni mwa wanawake wanaojua
kuchuna mabuzi.
Kauli hiyo imechochea vigezo vya kumfanya Shilole aonekane hasikii kwani
wiki kadhaa zilizopita mchungaji wa kanisa moja lililopo Ubungo, jijini
Dar ambaye hakujulikana jina lake, alimtaka kuishi katika sura ya
kumpendeza Mungu lakini inaonekana amempuuza.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko juzi, jijini Dar es Salaam, Shilole
alisema alitunga wimbo wa Nachuna Buzi kwa sababu anajua kuwa wanawake
wengi ni mafundi wa tabia hiyo akiwemo yeye mwenyewe!

0 Response to "JAMANI JAMANI HIVI SHILOLE ALIFIKIRIA NINI KUPOST PICHAZ ZA MAH*ABA KAMA HIZ MTANDAONI ?? JIONEE HAPA "
Post a Comment