Zuwena Yusuf Mohamed ‘Shilole.
MAMA wa majanga, Snura Antony Mushi kwa mara ya kwanza amejitokeza
hadharani na kuzungumzia kauli ya msanii mwenzake wa muziki wa mduara,
Zuwena Yusuf Mohamed ‘Shilole’ juu yake kuwa ameisha kimuziki ndiyo
maana ameamua kukimbilia muziki wa Taarab.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Snura ambaye anawika mitaani kwa ngoma kali kama Majanga na Nimevurugwa, alisema kitendo cha Shilole ‘kuponyokwa’ na maneno hayo ni ishara tosha kuwa anamkubali na kufuatilia kazi zake kwa ukaribu mkubwa.

Snura Antony Mushi.
“Sina tatizo na maneno ya Shilole, hiyo ni ishara kuwa anafuatilia na
kuzikubali sana kazi zangu, wala hawezi kunizuia kufanya kazi zangu kwa
namna ambavyo nafikiria, yeye afanye yake, nami nishike ‘hamsini
zangu’, alisema Snura.
0 Response to "SNURA AFUNGUKA , AMTUPIA MANENO SHILOLE NA HIKI NDICHO ALICHOKISEMA "
Post a Comment