MADEREVA WA MALORI WAFUNGA BARABARA BAADA YA WENZAO WATATU KUTEKWA NA KUCHARANGWA MAPANGA HUKO TABORA

IMG-20140126-WA0003
IMG-20140126-WA0006

 Taarifa zilizoufikia mtandao huu wa malunde1.blogspot.com asubuhi hii zinasema kuwa malori zaidi ya 40 yamezuia njia kufuatia tukio la kutekwa kwa madereva wenzao watatu wa malori na majambazi kisha kucharangwa mapanga,na inasemekana baada ya tukio hilo kutokea polisi walichelewa kufika eneo la tukio
.
Mbali na malori kuna Mabasi ya abiria na magari binafsi ambayo nayo hayawezi kupita kufuatia agizo la madereva hao ambao wamesema hawaachii njia mpaka Mkuu wa Mkoa wa Tabora au kamanda wa polisi mkoa wa Tabora  afike,huku wakidai kuwa eneo hilo limekua ni tatizo sugu kutokana na kutokea vitendo vya utekaji mara kwa mara.
Eneo hili linaitwa Iduguta mpakani mwa  eneo la Ziba ambalo lipo takribani kilomita 20 kutoka Nzega Mjini,madereva hao wa malori wameziba njia tangu saa 3 asubuhi hii,japo taarifa inasema tukio la kutekwa kwa madereva hao limetokea jana  saa 3 usiku.

0 Response to " MADEREVA WA MALORI WAFUNGA BARABARA BAADA YA WENZAO WATATU KUTEKWA NA KUCHARANGWA MAPANGA HUKO TABORA"

Post a Comment

wdcfawqafwef