Sehemu ya mlima unaolalamikiwa kumilikiwa na mwekezaji
Wananchi
wa kijiji cha Chalangwa Kata ya Chalangwa alfajiri majira ya saa kumi
wamefunga barabara ya Mbeya kwenda Chunya baada ya Jeshi la Polisi
kumkamata Mohammed Katembo kwa kosa la kutishia kuua.
Baada
ya kukamatwa Katembo nyumbani kwake baada ya kufungwa pingu akiwa
chini ya ulinzi akidai sababu za kukamatwa kwake ilipigwa mbiu kijijini
hali iliyopelekea wananchi kujitokeza kwa wingi na kuamua kuifunga
barabara hiyo huku mtuhumiwa akitoroka akiwa na pingu mkononi.
Hali
hiyo ilisababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo
wakiwemo abiria waliokuwa wanakwenda na kutoka mikoa ya kaskazini,huku
wananchi wakimtaka Mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro aje
kutatua mgogoro huo.
Mwenyekiti
wa kijiji Oscar Mwamwendesya amesema unatokana na mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina la Joseph Mwazyele kupora eneo la mlima katika
kijiji hicho bila taarifa ya uongozi wa kijiji kupitia mkutano mkuu wa
kijiji ambao ndio wenye dhamana ya kutunza raslimali za kijiji.
Mkuu
wa wilaya ya Chunya Deotatus Kinawiro alilazimika kuingilia kati na
kuifungua barabara hiyo majira ya saa nne na nusu asubuhi kisha kukutana
na wananchi wa Chalangwa ambapo aliwataka kutoa kero zao ili kuupatia
ufumbuzi mgogoro huo.
Wananchi
walidai kuwa Mwazyele amekuwa akitumia Polisi kwa kuwakamata wananchi
wanaohoji juu ya umiliki wa machimbo katika mlima kijijini hapo hivyo
wamekuwa wakiishi kwa hofu lakini pia hawjui uhalali wa umiliki wake kwa
kuwa kijiji hakina nyaraka zozote.
Katika
mkutano huo Mkuu wa Wilaya alipiga marufuku tabia za kujichukulia
sheria mkononi ikiwa ni pamoja na kufunga barabara na mauaji
yaliyokithiri kijijini hapo na wilaya ya Chunya kwa ujumla na Jeshi la
Polisi limekuwa likifanya kazi kubwa kudhibiti hali hiyo.
Aidha
amepiga marufuku shughuli zote za machimbo kijijini hapo na Mohammed
Katembo ajisalimishe na pingu za Polisi lakini wananchi walikataa
wakidai afunguliwe papo hapo ambapo Mtuhumiwa alijitokeza na kufunguliwa
pingu mbele ya Mkuu wa wilaya.
Mkuu
wa wilaya alimaliza kwa kuwataka wananchi kuchangia shilingi elfu mbili
kwa ajili ya uwanja wa kisasa wa michezo hali ambayo wananchi waliafiki
na kukubali kuchangia.
Na Ezekiel Kamanga
wa
Mbeya yetu
|
0 Response to "WANANCHI WAFUNGA BARABARA YA MBEYA CHUNYA BAADA YA MWENZAO KUKAMATWA / MTUHUMIWA AKIMBIA NA PINGU ZA POLISI "
Post a Comment