MBABE
wa zamani ulingoni, Frank Bruno amesema amerudi mazoezini tena, lakini
safari hii akijifua kuwa mtengeneza nywele za wanawake saluni.
Bingwa huyo wa zamani wa dunia wa nsonsi za kulipwa mwenye umri wa miaka 52 sasa alikumbana na suluba nyingi enzi zake ulingoni.
Lakini
baada ya msoto wa kutafuta msimamo mpya wa maisha tangu astaafu mwaka
1996, inatokea anataka kuhamishia umahiri wake wa ulingoni kwenye nywele
za mabinti.
Gwiji: Bruno akizipiga na bingwa mwingine wa zamani wa uzito wa juu, Mike Tyson ukumbi wa Hilton mjini Las Vegas mwaka 1989
Sura
ya maumivu: Bruno katika picha hii aliyopigwa Januari 2014 kwenye
shughuli ya hisani, sasa anaweza kuwa mtengeneza nywele wanawake saluni
Bruno
ametweet Ijumaa: "Ninajifunza hairdressing (utengenezaji nywele) wazo
lolote la jina la saluni? Itakuwa tayari miaka michache (ijayo),".
Mkazi
huyo wa London amekuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mtengeneza
nywele Nina Coletta ambaye ana saluni yake mjini Glasgow, na wawili hao
wamekuwa karibu mno na sasa anataka kufanya kazi pamoja naye.
Mwaka
2012 Bruno alikuwa akitibawa katika kliniki ya Glasgow na ndipo
alipokutana na Coletta katika harusi ya rafiki yake kwenye jiji hilo la
Scotland.
Katika
mahojiano aliyofanyiwa mwaka huo, Bruno alinukuliwa akisema:
"Amenisaidia kuliko uwezo wake. Namhitaji kuliko anavyonihitaji. Mwaka huu amenisaidia kutoka kwenye maradhi na kurudi katika uimara wangu,".
Bruno
amebaki kuwa mtu maarufu tangu astaafu ndondi na bado anapambana na
kumudu hali ya maisha nje ya ulingoni na aligundulika kuwa na maradhi ya
uchizi katika hospitali ya Mental Health Act mwaka 2003.
Bondia wa zamani, Bruno akiwa ameshika mwenge wa Olimpiki mjini London mwaka 2004
Bruno,
ulingoni akizipiga na Joe Bugner Uwanja wa White Hart Lane, enzi zake
alishinda mapambano 40 kati ya 45 aliyopigana, 38 kati ya hayo kwa
Knockout (KO).
0 Response to "UNAMKUMBUKA YULE BONDIA FRANK BRUNO...SASA NI MTENGENEZA NYWELE WANAWAKE SALUNI "
Post a Comment