Shule moja ya sekondari ya wasichana iliyopo wilayani Bagamoyo mkoani
Pwani, imelalamikiwa na wanafunzi pamoja na wazazi kuwa mabinti
wanajihusisha na vitendo vya ngono vya jinsia moja (usagaji).
Akizungumza na NIPASHE mmoja wa wazazi
(jina linahifadhiwa) alisema shule hiyo imepoteza sifa kwa kuwa kuna
wimbi kubwa la wanafunzi wanaojihusisha na vitendo hivyo vya usagaji.
Alisema mtoto wake alikuwa ameanza
kidato cha kwanza mwaka jana na baada ya kumuandikisha ndipo baadhi ya
watu walipomueleza kuwa shule hiyo kwa sasa ina sifa mbaya ya mchezo
‘huo mchafu.’
"Baada ya kuelezwa nikasema
nitalifanyia kazi jambo hilo hivi karibuni katika kupekua madaftari ya
mwanangu nakutana na kibarua cha mapenzi alichoandikiwa na msichana
mwenzake niliumia sana na nilitumia nguvu kumbana bila hivyo
asingeniambia," alisema
Alisema ilimbidi amhamishe binti yake
na kujiunga na shule moja ya sekondari iliyopo mkoani Tanga kwa ajili ya
kuendelea na masomo ya kidato cha pili mwaka huu.
Mzazi huyo alisema anashangazwa ni kwa
nini hatua hazichukuliwi wakati suala hilo ni la hatari kwani watoto wao
wataharibika kiakili pamoja na kimwili na wanaweza kuambukizana VVU na
Ukimwi..
Alisema wakati mwanaye akisoma katika
shule hiyo alikuwa akihudhuria vikao vya wazazi mara kwa mara na kwamba
kila kikao walikuwa wakifukuzwa wanafunzi kutokana na mwenendo huo.
"Hili tatizo ni kubwa na kufukuzwa kwa
mwanafunzi sidhani kuwa wanatatua tatizo nadhani hakuna usimamizi mzuri
kwani wangeweza kudhibiti kwa haraka tatizo hilo kabla ya kuwa kubwa,"
alisema
Pia alisema ndugu yake imembidi
amhamishe mwanae na kumtafutia shule nyingine kwa kuhofia binti yake
kurubuniwa kwani wanakuwa ni wadogo na hawaelewi chochote, hivyo inaweza
kuwa rahisi kudanganywa na kuingia kwenye vitendo hivyo viovu.
Alisema kuwa hata kiwango cha ufaulu kwa sasa shule hiyo imeshuka kutokana na tatizo hilo kwa wanafunzi .
Hata hivyo, NIPASHE ilizungumza na
mwanafunzi mmoja ambaye anasoma katika shule hiyo kuhusiana na suala
hilo ambapo alikiri kuwepo kwa jambo hilo na kueleza kuwa wanaofanya
mchezo huo ni wa kidato cha tano na cha sita.
"Mimi hawajanifanyia ila najua wanaofanya mchezo huo ni wale walioko kidato cha tano na cha sita," alisema Pia kuna baadhi ya wazazi wengine wamekuwa wakilalamikia jambo hilo na kueleza kuwa ndugu zao imewalazimu kuwahamisha watoto wao kutokana na vitendo hivyo vinavyofanyika shuleni hapo
0 Response to "UGONJWA WA MAPENZI YA JINSIA MOJA WAINGIA HADI MASHULENI.TAZAMA PICHA ZA WANAFUNZI WALIVYO FUMANIWA WAKIFANYA MAPENZI YA NJIA MOJA "
Post a Comment