Jiji la dar es salaam huwa ni tamu lakini lina kero
zake na uenda kero ni nyingi kuliko raha zilizopo… moja wapo ya kero
kubwa zaidi ni hili ambalo bila shaka kila mmoja wetu anayeishi
uswahilini linamgusa kwa namna moja ama nyingine … si linguine ni swala hili la miziki ya kukesha ambayo imejichukulia
umaarufu kwa jina la vigodoro, kwa mtu anaye kaa mitaaa ya mbezi beach,
upanga au masaki ni vigumu kuelewa nachomaanisha lakini kwa watu wa
yombo vituka, tandale kwa tumbo , ukonga mazizini na sehemu kama tandika
wananielewa vizuri…
crdt
gumzo la jiji
Ni ukweli usiopingika kuwa hii ni
kelo ya watanzania wengi hapa jijini, mara nyingi miziki hii uanza siku
ya alhamisi au ijumaa na kwenda mpaka jumapili… kero hii inatokana na
mtindo wa upigaji wa mziki huu usiozingatia mda ambapo upigwa mpaka
asubuhi bila kujali usumbufu mkubwa wanoupata watu wa karibu na vigodoro
hivyo…sasa pata picha umerudi toka kazini sa tano usiku kutokana na
foleni iliyopo mjini na unaamua kujipumzisha kidogo ili uwahi kuamka
ukatafute riziki… kwa sauti ya mziki huu sidhani kama utapata usingizi …
kitu ambacho kinaweza kupelekea uamke umechoka na ushindwe kufanya kazi
zako kwa ufasaha,,,, hapa tunaweza kusema kwamba miziki hii inarudisha
nyuma maendeleo ya watanzania nan chi kwa ujumla. Kero
nyingine ya miziki hii ya usiku ni ukiukwaji wa maadili ya mtanzania
kwani kubali ukatae watu wanacheza bila kuhofia chochote na mara nyingi
kama unavyojua nyumba zetu za uswahilini wengi hatuna mageti ya kuwazuia
watoto wetu… watoto wengi wa umri wa chini ya miaka kumi na nane
wamekuwa wakitoroka nyumbani na kukimbilia kwenye vigodoro hivo na
kuwafanya wajifunze tabia ambazo ni zaidi ya umri wao.
Nadhani imefika wakati sasa
serikali kuangalia upya sharia za upigaji mziki katika kumbi za starehe
na majumbani.. mara nyingi sharia inasema baa zifungwe sa sita labda uwe
na kibali naalum kutoka sehemu husika .. lakini hii imekua ni tofauti
kwa vigodoro kwani uenda mpaka asubuhi na kusababisha kero isiyokuwa ya
kawaida kwa wakazi wa maeneo ya uswahilincrdt
gumzo la jiji
0 Response to "Tazama Vigodoro vya Uswahilini, Ngono Nje Nje…!! "
Post a Comment