Imeelezwa kwamba habari hiyo ilianzia kwenye mtandao mmoja wa nchini Marekani itwao Abril Uno, ambao uliandika habari hiyo wiki iliyopita siku ya Jumatano.
Kwenye tarifa yake mtandao huo ulitania kwa kuandika kwamba Diana Kamuntu, mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amejitangaza kuwa ni msagaji kwenye mahojiano na kituo kimoja cha redio.
Taarifa hiyo ilisema: “Mimi ni msagaji, ninafanya mapenzi ya jinsia moja. Nimelijua hilo toka nilivyokuwa msichana mdogo,” taarifa ilimnukuu Kamuntu.
Kwenye mtandao wa Abril Uno ulimtaja muendesha kipindi wa redio hiyo James Kasirivu, kuwa ndiye aliyekuwa akifanya mahojiano hayo, na kusema kwamba “alipatwa na mshangao na mpaka aliishiwa na maneno ya kuongea toka kinywani mwake.”
Maelezo hayo yalisambaa kwenye mitandao mingi Duniani, huku wengine kuitoa na wengine kuiacha.
Watu wengi waliguswa na taarifa hiyo huku baadhi yao wakiandika kwenye kurasa zao za Twitter katika hali ya kumuunga mkono Kamuntu:
0 Response to "OOOH..KUHUSUI BINTI WA RAISI MUSEVEN WA UGANDA KUKIRI KUWA NI MSAGAJI...!JIONEE MWENYEWE UKWELI HAPA... "
Post a Comment