Mwanamke Huyu Khaaaa...Nahisi Nabambikiwa Live Live..Kaniona Zoba,,,,,SOMA NA TOA USHAURI


Jamani naleta hili tatizo nipeni mawazo yenu,
Mwezi Novemba mwaka jana nilikutana na binti mmoja. Alitokea kunipenda ghafla lakini mimi sikuwa na mawazo hata. Nilivyoona ananisumbua na sms zisizokoma nikaamua nile mzigo ila
tulitumia kinga mwanzo mpaka mwisho. Basi tukaachana hatukukutana tena mpaka leo. Mwezi huu wa tatu mwanzoni akanipigia na kuniambia ana mimba yangu. Nikashangaa, nilischofanya ni kumhoji akagoma akasema kwa vyovyote itakuwa yangu. Nikamwambia mbona hukuniambia tangu Novemba mpaka leo ni miezi mitano, akasema alikuwa anatafuta nafasi aniambie akawa anakosa chance. Nikajua ananizuga au anataka kunibambika. Nikamwambia ok, kama ni hivyo ilee hiyo mimba utakapojifungua niko tayari tukapime DNA uwe tayari kupokea majibu, kama siyo yangu ujue ntakachokufanyia nitajua mwenyewe. Akasema sawa. Wiki hii amenipigia simu kuwa mimba imeharibika anataka nimpe hela kwa sababu anaumwa na anataka akasafishe. Pia anataka hela ya matumizi mara ananiambia mambo ya huko kwao. Agenda sasa imebadilika kutaka hela.

Sasa kinachonishangaza ananiambia mambo short cut, hakuna maelezo. Hivi si kashapoteza ushahidi, na mimi sitaki anavyonisumbua, nifanyeje?

0 Response to "Mwanamke Huyu Khaaaa...Nahisi Nabambikiwa Live Live..Kaniona Zoba,,,,,SOMA NA TOA USHAURI "

Post a Comment

wdcfawqafwef