Sunday, 23 March 2014
HIZI NDIZO AINA YA VYAKULA VINAVYOONGEZA UWEZO KATIKA TENDO LA NDOA YAANI KUIMARISHA UME WAKO
.
Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni mwa wanandoa na wapenzi wengi,Tatizo hili lipo kwa wanaume kwa kiasi kikubwa na wanawake pia,hapa nitaelezea baadhi ya vyakula ambavyo husaidia kuongeza uwezo ktk tendo.
1: PARACHIHI.
Tunda hili lina uwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E ambayo husaidia ktk uzalishaji wa homoni.Inatajwa kuwa watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwa na msisimko mkali wa kimapenzi na kwa wanawake husaidia kuongeza majimaji yenye utelezi sehemu za siri na hivyo kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa kujamiiana.
2:NDIZI.
Wakati unafikiria uwezo wa kufanya vema tendo la ndoa,unatakiwa kuwaza juu ya uimara wa misuli ya mwili ambayo inatajwa kuwa ni sehemu kuu na yenye umuhimu ktk kujamiiana.Kwa msingi huo ulaji wa ndizi mbivu unatajwa kusaidia kujenga misuli mwilini na kumfanya mtu aweze kuwa hodari ktk tendo la ndoa.
3: CHOKOLETI.
Ulaji wa chokoleti huongeza uchangamfu mwilini na hivyo kumuwezesha mtu anayeshiriki tendo la ndoa kuwa na mguso sahihi kwenye fikra zake,jambo litakalomwezesha kupokea hisia za mapenzi kwa urahisi zaidi ya mtu anayekwenda kwenye uwanja wa sita kwa sita akiwa mchovu wa mawazo.
4: VANILA.
Vanila husaidia kuamsha hamasa mwilini.Aina hizi ya vyakula inatajwa kuwa na virutubisho vingi vyenye uwezo wa kuusaidia mwili kuwa na nguvu za kutosha kufanya tendo la ndoa.
5: MBEGU ZA MATUNDA.
Mchanganyiko wa mbegu mbalimbali za matunda husaidia kuondoa ACID mwilini na kumfanya mtu ajione ni mwenye afya njema.
6: POMEGRANATE.
Ni aina fulani ya matunda mekundu yanayofanana na apple.Haya yanatajwa kusaidia kuamsha mishipa ya fahamu na kuweka mawasiliano sahihi ya mwili na hivyo kumuongezea mtu uwezo wa kufanya tendo la ndoa kwa hamasa kubwa.
7: MVINYO MWEKUNDU.
Mvinyo mwekundu unatajwa kuwa na uwezo wa kuuchangamsha mwili na kuongeza msukumo wa damu kiasi cha kumuondolea mtu uchovu kabla na baada ya tendo la ndoa,hivyo ni muhimu kunywewa hasa na wale ambao wanasumbuliwa na tatizo ia kushindwa kurudia tendo.
8: CHAZA NA PWEZA.
Aina hizi za samaki huwa na madini ya Zink na chumvi ambayo yanatajwa kusaidia uzalishaji wa vichocheo vinavyohamasisha msisimko wa mwili wakati wa tendo la ndoa.
TUJIHADHARI NA UTUMIAJI WA MADAWA YA KUONGEZA NGUVU ZA KUFANYA TENDO KWANI SI MAZURI KWA AFYA.
0 Response to "HIZI NDIZO AINA YA VYAKULA VINAVYOONGEZA UWEZO KATIKA TENDO LA NDOA YAANI KUIMARISHA UME WAKO"
Post a Comment